1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roma: Rais George W. Bush wa Marekani ziarani Italia.

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtU

Rais George W. Bush wa Marekani amewasili nchini Italia kwa mashauriano na waziri mkuu wa nchi hiyo, Romano Prodi na pia kiongozi wa kanisa katoliki, Papa Benedikti wa kumi na sita.

Maafisa wa serikali ya Italia wanasema wanatarajia maandamano na ghasia zitazuka kutokana na ziara hiyo ya siku moja ya Rais George Bush.

Baadhi ya wabunge wa serikali ya mseto ya Romano Prodi wamesema huenda watashiriki maandamano hayo.

Rais George Bush anaitembelea Italia wakati ambapo kesi imeanza mahakamani dhidi ya majasusi wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA , wanaoshutumiwa kwa kumteka nyara mtu aliyeshukiwa kwa vitendo vya ugaidi.

Kiongozi huyo wa Kiislamu alitekwa nyara katika mji wa Milan na kupelekwa katika gereza moja nchini Misri anakodai aliteswa.

Rais George Bush amewasili nchini Italia kutokea Poland alikoshauriana na rais wa nchi hiyo kuhusu ujenzi wa kituo cha kukinga makombora katika eneo la Ulaya mashariki.