1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Prodi akaribia kurejea wadhifa wake

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPI

Romano Prodi anakaribia kurejea katika wadhifa wake wa waziri mkuu wa Italia baada ya kupata uungwaji mkono na serikali yake ya mseto ya mrengo wa kati na kushoto.

Rais wa Italia, Giorgio Napolitano, anaendelea na mazungumzo kujaribu kuutanzua mzozo wa kisiasa nchini humo. Atanatakiwa kuamua ikiwa waziri mkuu Prodi au kiongozi mwengine ataunda serikali mpya ya mseto au aitishe uchaguzi mpya nchini Italia.

Romano Prodi alijiuzulu juzi Jumatano baada ya serikali yake ya mseto kushindwa kwenye kura iliyopigwa bungeni.

Mswada uliopigiwa kura ulihusu mpango wa kurefusha muda wa wanajeshi 2,000 wa Italia walio nchini Afghanistan na upanuzi wa kambi ya jeshi la Marekani katika mji wa kaskazini wa Vicenza.