1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH : Cheney akutana na Mfalme Abadullah

Makamo wa rais wa Marekani Dick Cheney yuko nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo na Mfalme Abdullah.

Cheney amewasili katika mji wa kaskazini wa Tabuk na anatarajiwa kujadili na mfalme huyo kuongezeka kwa nguvu ya Iran katika Mashariki ya Kati.Katika ziara yake ya wiki moja katika eneo hilo Cheney amekuwa akijaribu kuzishawishi nchi marafiki wa Marekani zilioko Mashariki ya Kati kusaidia kuwavuta Waislamu wa madehebu ya Sunni walio wachache nchini Iraq kujiunga na mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo.

Vita nchini Iraq vimedhoofisha uhusiano mzuri kati ya Marekani na Saudi Arabia.

Mwezi wa Machi uliopita Mfalme Abdullah aliiufunguwa mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Kiarabu mjini Riyadh kwa hotuba ilioshutumu kukaliwa Iraq kwa mabavu na wageni kusiko halali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com