1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Vita vya Gaza

Munira Muhammad30 Januari 2010

Israel na Palestina wawasilisha maelezo yao kuhusu vita vya muda mfupi huko Gaza mwanzoni mwa mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/LnWR
Jaji Richard Goldstone, Afisa wa Umoja wa Mataifa aliyechunguza vita huko Gaza.Picha: AP / United Nations



Israel na Mamlaka ya Palestina zimewasilisha maelezo yao kwenye Umoja wa Mataifa kuhusiana na ripoti ya vita vya Gaza mwanzoni mwa mwaka uliopita. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon sasa ana muda wa hadi Ijumaa ijayo kutathmini maelezo ya pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa mchunguzi wa Umoja wa Mataifa, Richard Goldstone nchi zote mbili zilihusika na makosa ya uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binaadamu. Kama ilivyotarajiwa, maelezo ya Israel yaliikosoa ripoti ya Goldstone kwamba inapotosha, ya uongo na inakosa uwajibikaji.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Palestina ilikataa kutoa maelezo juu ya ripoti yake, ikisema kuwa ni ya siri na kwamba ni jukumua la mkuu wa Umoja wa Mataifa kuamua kama yawekwe wazi au la. Ripoti ya Goldstone inaeleza kuwa mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas, yaliwaua Wapalestina 1,400 na Waisrael 13.