1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Ubalozi wa Marekani, Benghazi

19 Desemba 2012

Ripoti ya Uchunguzi kuhusu shambulizi kali lililofanywa na wamgambo dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Libya, Benghazi, imeishutumu mipangilio ya usalama ya wizara ya mambo ya kigeni katika ubalozi huo

https://p.dw.com/p/175HL
Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service The U.S. Consulate in Benghazi is seen in flames during a protest by an armed group said to have been protesting a film being produced in the United States September 11, 2012. An American staff member of the U.S. consulate in the eastern Libyan city of Benghazi has died following fierce clashes at the compound, Libyan security sources said on Wednesday. Armed gunmen attacked the compound on Tuesday evening, clashing with Libyan security forces before the latter withdrew as they came under heavy fire. REUTERS/Esam Al-Fetori (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)
Libyen Bengasi Anschlag auf US-KonsulatPicha: Reuters

Ripoti hiyo imesema usalama haukuwa wa kutosha kabisa pamoja na mbinu duni kuweza kukabiliana na mashambulizi ya aina hiyo. Uchunguzi huo uliochukua miezi kadhaa pia umebainisha kwamba hakukuwa na ujasusi wa aina yoyote maalum wa kitisho dhidi ya ubalozi huo, ambao ulivamiwa mnamo tarehe 11 Septemba na wanamgambo waliokwua na silaha na ambao waliwauwa Wamarekani wanne ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini humo. Ripoti hiyo iliyotolewa na Bodi ya Tathmini ya Uwajibikaji pia imesema kwamba hakukuwa na maandamano yoyote kabla ya mashambulizi hayo, ambayo hayakutarajiwa katika kiwango cha ukubwa wake.

Mashambulizi hayo ambayo ubalozi huo mdogo pamoja na ofisi yingine zilizokuwa karibu zililengwa, yamezusha mdahalo mkali wa kisiasa, huku Warepublican wakiushambulia utawala wa Marekani kwa kukosa kuwajibika kiusalama, pamoja na uwezekano wa kuficha ukweli kuhusu jukumu la kundi la Al-Qaeda.

Aliyekuwa balizi wa Marekani mjini Benghazi J. Christopher Stevens
Aliyekuwa balizi wa Marekani mjini Benghazi J. Christopher StevensPicha: AP

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, amejikuta akizongwa na mashambulizi makali ya Warepublican kwa kusema siku chache baada ya shambulizi hilo kwamba, kulingana na ripoti za ujasusi, shambulio hilo lilichochewa na maandamano ya ghafla nje ya ubalozi huo. Rice hivyo amelazimika kujiondoa kutoka kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Waziri wa Mambo ya Kigeni Hillary Clinton, ambaye anawacha wadhifa huo mapema mwaka ujao.

Juhudi zilifanywa kumwokoa balozi

Katika sehemu moja ya ripoti hiyo ambayo haijawekwa siri, bodi hiyo yenye wanachama watano imesema inaamini kila juhudi zilifanywa kumwokoa balozi Chris Stevens, ambaye aliiaga dunia katika shambulizi hilo, akiwa ni balozi wa kwanza wa Marekani kuuwawa akiwa kazini baada ya kupita miongo mitatu. Bibi Clinton amesema amekubali kila moja ya mapendekezo 29 yaliyotolewa na bodi hiyo ya uchunguzi ambayo imetumia miezi mitatu kuchunguza matukio hayo. Pia amesema kwamba Wizara ya Mambo ya Nje inashirikiana na Wizara ya Ulinzi ili kuwatuma mamia ya walinzi wengine wa kijeshi kuimarisha balozi za nchi za Marekani, na kwamba wanalenga kuwapa mafunzo ya usalama maafisa wa kidiplomasia.

Clinton amewaambia wabunge kupitia barua aliyowatumia kwamba ijapokuwa kila mtu katika wizara hiyo alikuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa wanadiplomasia hao, kwa kiwango kikubwa lilikuwa ni jukumu lake kama Waziri wa mambo ya kigeni. Ameyaunga mkono matokeo ya ripoti hiyo na kutoa wito kwa Bunge kuunga mkono ombi la bajeti ya mwaka wa 2013 ya wizara hiyo ili kusaidia kumarisha vituo vyote vya kidiplomasia.

Hi ni baada ya ripoti hiyo kusema kwamba maombi ya kila mara ya kupatiwa msaada zaidi yaliyotolewa na wafanyakazi wa ubalozi mjini Benghazi na mji mkuu wa Libya Tripoli yalipuuzwa, ikiongeza kuwa ubalozi maalum wa Benghazi haukupewa kipau mbele na serikali ya Marekani mjini Washington. Lakini ikasema balozi Stevens alifanya uamuzi wa kwenda Benghazi kibinafsi, kama jukumu la kawaida, na kwa sababu aliifahamu kwa undani Libya, serikali ya Washington ilitoa mtazamo tofauti kwa maamuzi yake. Clinton sasa amempa jukumu msaidizi wakeTom Nides kuongoza kundi ambalo limekutana kwa mara ya kwanza leo, kutekeleza mapendekezo ya ripoti hiyo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Hamidou Oummilkheir