Rio De Janeiro. Hakuna matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rio De Janeiro. Hakuna matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai.

Maafisa wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini Brazil wamesema kuwa hakuna matumaini ya kuwapata watu walionusurika kutoka katika ndege ambayo imeanguka katika msitu wa Amazon nchini humo.

Taarifa hiyo inakuja saa chache baada ya jeshi la anga la Brazil kugundua sehemu ndege hiyo ya abiria ilipoangukia katika eneo la jimbo la Mato Grosso.

Ndege hiyo mali ya shirika la ndege la binafsi la GOL ilikuwa imebeba abiria 115 kutoka katika mji wa Manaus ikiwa inakwenda katika mji mkuu Brasilia wakati wadhibiti wa safari za anga walipopoteza mawasiliano na marubani wa ndege hiyo.

Sababu za kuanguka kwa ndege hiyo hazijafahamika lakini maafisa wanasema wanaamini inaweza kuwa ndege hiyo iligongana na ndege ndogo ambayo ilifanikiwa baadaye kutua salama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com