1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rice mashariki ya kati kuanzia ajumatatu

Hamidou, Oumilkher23 Agosti 2008

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ataka kuhimiza makubaliano ya amani kati nya Israel na Palastina

https://p.dw.com/p/F3by

Washington:


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani,bibi Condoleezza Rice anapanga kuzitembelea Israel na maeneo ya utawala wa ndani wa Palastina jumatatu ijayo.Lengo la ziara yake ni kuwahimiza waisrael na wapalastina wafikie makubaliano ya amani hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu.Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Washington.Condoleezza Rice atakutana na viongozi wa Israel na Palastina,amesema hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje,Sean McCormack,bila ya kufafanua.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice anataka pia aarifiwe juu ya mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa Annapolis Marekani,mwezi November mwaka jana.Mazungumzo hayo yanazungumzia uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya amani kabla ya kumalizika mwaka huu wa 2008.