Riadha kuanza Beijing | Michezo | DW | 13.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Riadha kuanza Beijing

Baada ya macho kukodolewa katika hodhi la kuogolea,kuanzia ijumaa bunduki italia kuwaita wanariadha na hasa waafrika.

default

Mjerumani Hinrich Romeike, )

Leo ni siku ya 6 ya michezo ya olimpik ya Beijing na mashabiki wa Afrika wakisubiri kwa hamu kuu kuwaona wanariadha wao wakiteremka uwanjani na kutamba kuanzia mbio za masafa ya kati ya mita 800 hadi masafa marefu -marathon ambamo mkenya Cathrine Ndereba, ndie bingwa wa dunia na wa Boston marathon.

Ijumaa, bunduki italia kuanzisha changamoto ya mita 100 wanaume ambayo finali yake itakua jumamosi kuamia binadamu wa kasi kabisa kati ya Muamerika mmoja-bingwa wa dunia Tyson Gay na wajamaica 2 bingwa wa rekodi ya dunia wa sasa na wa zamani Usain bolt na Asafa Powell.

Katika masafa ya kati na marefu mita 1500 na mita 5000,mzaliwa wa Kenya anaepepea bendera ya Marekani Bernerd Lagat anapanga tena kuwatilia wakenya kitumbua chao mchanga katika masafa hayo 2 .Lagat alifanya hivyo katika mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia mwaka jana huko Osaka,Japan.

Ingawa Lagat amezaliwa Kenya na miaka ya nyuma akikimbia chini ya bendera ya Kenya, anasema, "Ninajivunia kuwa sehemu ya Marekani."

katika michezo hii ya Beijing, Lagat analenga shabaha sawa na ile aliolenga Osaka,Japan mwaka jana:kushinda tena mbio za mita 1.500 na mita 500 wanaume.huu ni ushindi alioleta mwanariadha mmoja tu kabla yake-stadi wa Finland marehemu Paavo nurmi.

kikosi cha Kenya nacho kimejiandaa kwa changamoto zinazoanza ijumaa na hasa katika mbio za mita 800 wanawake, mita 3000 kuruka viunzi na mbio za marathon.Mahasimu wao wakubwa wakenya, ni jirani zao Ethiopia na hasa akina Dibaba na Kenenisa Bekele: