1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RI-KWANGBA: Jan Egeland amekutana na viongozi wa LRA

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtQ

Mkuu wa miradi ya kiutu ya Umoja wa Mataifa,Jan Egeland,amewasili nchini Sudan kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la Uganda,LRA.Ripoti zinasema,Egeland amekutana pia na Joseph Kony katika eneo la msituni lililo kati ya mpaka wa kusini wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako viongozi wa ngazi ya juu ya LRA wana makao yao. Joseph Kony ni miongoni mwa washukiwa wanaosakwa na jumuiya ya kimataifa kuhusu uhalifu wa vitani.