1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Reid amtaka Bush kuzingatia sera kuelekea Pakistan

Abdulrahman, Mohamed11 Januari 2008

Pakistan imeukataa wito wa Kiongozi wa maseneta wa Wademokrats wenye wingi katika baraza hilo Harry Reid, kumtaka Rais George W. Bush azingatie kupunguza msaada kwa Pakistan.

https://p.dw.com/p/CoJu
Seneta Harry ReidPicha: AP

Bw Reid ambaye ni seneta mdemokrat kutoka jimbo la Nevada, alimwambia Rais Bush katika barua kwamba mauaji ya kiongozi wa upinzani Bibi Benazir Bhutto wiki mbili zilizopita, yameongeza wasi wasi juu ya hali ya baadae ya Pakistan, na utendaji wa Rais Pervez Musharraf.


Seneta huyo ambaye ametaka sera kamili ya Marekani ipitiwe upya baada ya Musharraf kutangaza sheria ya hali ya hatari mwezi Novemba, alisema Rais Bush hana budi kuweka masharti kwa msaada wa Marekani kwa Pakistan, chini ya zingatio la kuwepo kwa haki kamili za kiraia ambazo bado zimeekewa mipaka, licha ya kuondolewa sheria ya hali ya hatari.


Seneta Reid akamtaka Musharraf arejeshe uhuru wa vyombo vya habari na haki ya aqwatu kujumuika, awaachie huru wafungwa wa kisiasa waliokamatwa wakati wa msako uliotokana na hatua hiyo, kuwarudisha kazini majaji aliowafukuza mwezi Novemba na aunge mkono uchunguzi wa umoja wa mataifa kuhusiana na mauaji ya bibi Bhutto.


Lakini mseamaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Pakistan Mohammad Sadig amesema hapapaswi kuwekwa masharti katiaka kile alichokiita " uhusiano muhimu sana" kati ya nchi hizo mbili.

Akaongeza kwamba wanaamini masharti yoyote yatakayoambatanishwa katika uhusiano huo au msaada hayyatokua na manufaa. Akasema kwa upande wa Pakistan haittochukua uamuzi kwa sababu mtu fulani ameadai iwe hivyo bali uamuzi wowote utachukuliwa kulingana na sheria za nchi hiyo na hali halisi ya nchi hiyo.


Pakistan , dola yenye nguvu za nuklea imepokaea kiasi ya dola bilioni 10 za kimarekani kama msaada tangu 2001, wakati Pakistan ilipoacha kuwaunga mkono Wataliban katika nchi jirani ya Afghanistan na kujiunga na vita vinavyoongozawa na Marekani dhidi ya ugaidi, baada ya matukio ya Septemba 11 katika ardhi ya Mareakani.


Lakini hatua ya kiongozi wa Pakistan kutangaza sheria ya hali ya hatari Novemaba 3, ililisababisha bunge la Marekani kushurutisha masharti fulani yaambatanishwe na masuala ya demokrasia na viata dhidi ya ugaidi katika msaada utakaotolewa kwa Pakistan.


Mswaada wa sheria unaohusiana na bajeti ukazuwia dola milioni 50 kati ya 300 milioni za msaada wa kijeshi kwa Pakistan hadi Waziri wa mambo ya nchi za nje Condoleezza Rice atakaporipoti mbele ya bunge hilo, kuwa Pakistan imerejesha haki za demokrasia na uhuru wa vyombo vya kisheria, pamoja na kuongeza juhudi katika kupambana na al Qaeda na wanaharakati wa Kitalibani.


Wabunge awa Marekani wakapitisha uamuzi kuwa dola 250 milioni zilizosalia, zitumike tu kama msaada wa kijeshi katika kupambana na ugaidi au kuimarisha sheria dhidi ya harakati wa al Qaeda na watalibani.


Pakistan imegeuka kuwa mada muhimu nchini Marekani, katika wakati ambao wanasiasa wanashiriki katika hatua za mwanzo za uchaguzi ndani ya vyama vyao, kuelekea uchaguzi wa Rais mwezi Novemba.


wanasiasa wa Marekani wamezusha hofu walionazo kuhusiana na silaha za kinuklea za Pakistan kuweza kuangukia mkononi mwa wanaharakati. licha ya kwamba maafisa wa ulinzi wa Marekani wanasema silaha hizo ziko salama. zikidhibitiwa na jeshi la Pakistan.

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani pia wametoa wito wa hujuma za kijeshi dhidi ya wanaharakati ndani ya Pakistan.


Lakini matamshi hayo yamejibiwa na rais musharraf katika mahojianop na gazetzi moa la Singapore" Times" akisema hatua yoyote ya upande mmoja itakayoongozwa na Marekani dhidi ya wanaharakati katika eneo la mpaka na Afghanistan, litachukuliwa kuwa ni uvamizi. Akasema,yeyote atakayekuja katika milima yetu atajuta. Pakistan inahofia hatua zozote za kuruhusu majeshi za kigeni kuendesha harakati katika ardhi zake katika mpaka na Afghanistan, itachochea mripuko na ula paji kisasi kutoka kwa watu wa kabila la Pashtun katika eneo hilo.