1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real kukwaana na Bayern; Robo fainali Ulaya

17 Machi 2017

Mabingwa watetezi  wa kombe la mabingwa Ulaya, Real Madrid watakabiliana na Bayern Munich chini ya kocha wao wa zamani Carlo Ancelotti katika mechi za Robo fainali, za ligi ya Mabingwa barani Ulaya

https://p.dw.com/p/2ZPPZ
UEFA Champions League
Picha: Getty Images/R. Heathcote

Mechi hizo zitachezwa kati ya april 11 na 18.

Magwiji wa soka wa Italia Juventus, wanataraji kulipiza kisasi kwa mahasimu wao waliowaangusha kwenye fainali hizo mwaka 2015 Barcelona ya Uhisapania, lakini bado watakabiliwa na kazi kubwa ya kumzima mchezaji hatari kwenye michuano hiyo Lionel Messi.

Mabingwa wa ligi ya England, ambao si wazoefu kwenye michuano hiyo Leicester wanakutana na Atletico Madrid. Monaco ambayo kwa msimu huu imefunga mabao mengi itakutana na Borussia Dortmund huku Bayern Munich mabingwa wa mwaka 2012 wakiwakaribisha mabingwa wa mara kumi na moja Real Madrid katika mechi ya mkondo wa kwanza wanapolenga kutinga nusu fainali kwa mara ya sita mfululizo.

Mwandishi: Lilian Mtono.

Mhariri:Iddi Ssessanga