1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rangoon. Utawala wa kijeshi waondoa majeshi yake mitaani.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HZ

Utawala wa kijeshi wa Burma umesema kuwa umeondoa vikosi vyake vya jeshi kutoka katika mitaa ya mjini Rangoon na kuwaacha huru wengi wa wanaharakati waliokamatwa katika ukandamizaji na kuvunjwa kwa maandamano ya kudai demokrasia.

Wakati huo huo , utawala huo wa kijeshi umesema kuwa umewakamata watu wengine zaidi na kukamata idadi kubwa ya silaha kutoka kwa watawa wa Kibudha. Taarifa hiyo , ambayo imechapishwa katika gazeti la mjini Rangoon , imekuja muda kabla ya mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya iwapo baraza hilo liidhinishe waraka juu ya muswada unaozungumzia juu ya mzozo huo , waraka uliotayarishwa na Uingereza, Ufaransa na Marekani. Pendekezo hilo linashutumu ukandamizaji wa nguvu dhidi ya maandamano ya amani, na kuwataka majenerali watawala nchini Burma kuwaacha huru wafungwa wote wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi.