RANGOON: Suu Kyi akutana na mjumbe wa utawala wa kijeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RANGOON: Suu Kyi akutana na mjumbe wa utawala wa kijeshi

Kiongozi wa upinzani,Aung San Suu Kyi amekutana na afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya kijeshi ya Burma.Televisheni ya taifa imethibitisha kuwa Suu Kyi alie na kifungo cha nyumbani,aliruhusiwa kutoka nje ya nyumba yake kwenda kukutana na jemadari mstaafu Aung Kyi.

Mapema mwezi huu,mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari alitoa mwito kwa utawala wa kijeshi wa Burma,kumteua afisa wa kuanzisha majadiliano pamoja na wapinzani.Gambari alikwenda Burma baada ya utawala wa kijeshi kutumia nguvu dhidi ya watawa wa Kibudha na raia walioandamana mwezi uliopita kuunga mkono udemokrasia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com