1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Kiongozi wa upinzani kukutana na watawala wa kijeshi

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78n

Kiongozi wa upinzani nchini Burma,Aung San Suu Kyi yupo tayari kujadiliana na watawala wa kijeshi nchini humo.Katika taarifa iliyosomwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Ibrahim Gambari,kiongozi huyo wa upinzani amesema,anachukua hatua hiyo kwa maslahi ya umma. Utawala wa kijeshi unatazamia pia kumruhusu mshindi huyo wa zawadi ya amani ya Nobel, kukutana na viongozi wa chama chake kinachogombea demokrasia.Aung San Suu Kyi tangu miongo kadhaa, yupo katika kizuizi cha nyumbani.