RAMALLAH:Rais Abbas kutoa wito wa uchaguzi wa mapema | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH:Rais Abbas kutoa wito wa uchaguzi wa mapema

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatoa wito wa kufanywa uchaguzi wa mapema.Mpango huo unapingwa na chama cha Hamas kinachomiliki Ukanda wa Gaza.

Katika hotuba mjini Ramallah Bwana Abbas alisema kuwa uchaguzi wa mapema wa wabunge na rais unapangwa kufanyika ila hakutoa tarehe rasmi.Baraza kuu la Uongozi la Palestinian Liberation Organisation, PLO linatarajiwa kushughulikia wito huo hii leo.Mwezi jana Rais Mahmoud Abbas alivunja serikali ya kitaifa iiliyoongozwa na chama cha Hamas chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu wa zamani Ismail Haniyeh.Hayo yalitokea baada ya Hamas kuteka Ukanda wa Gaza.Rais Abbas aliunda serikali mpya iliyo na wafuasi wengi wa chama chake cha Fatah.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com