1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleeza Rice, aendelea na ziara yake Mashariki ya Kati.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCal

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleezza Rice amewasili mjini Ramallah kushauriana na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas katika siku ya pili ya ziara yake ya juma moja Mashariki ya Kati.

Bi Condoleezza Rice jana mjini Jerusalem alishauriana na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israil Tzipi Livni ambapo alitoa wito wa kuwa na suluhisho mwafaka la mzozo kati ya Israil na Wapalestina.

Marekani imekuwa ikishinikizwa na washirika wake kutoka Ulaya na pia mataifa ya Kiarabu kufufua mashauriano ya amani ya Mashariki ya Kati.

Baadaye hivi leo, Bi Condoleezza Rice anatarajiwa kuitembelea Jordan kabla ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert kesho.