1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice ashauriana na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCac
Marco kijana wa kijerumani anayezuiliwa nchini Uturuki
Marco kijana wa kijerumani anayezuiliwa nchini UturukiPicha: picture-alliance/ dpa

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Condoleezza Rice, ameshauriana na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas mjini Ramallah katika siku ya pili ya ziara yake ya juma moja Mashariki ya Kati.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mashauriano kati yake na Rais Mahmoud Abbas, Bi Condoleezza Rice, amesema Marekani imejitolea kutanzua mzozo kati ya Israil na Palestina.

Naye Rais Mahmoud Abbas, ametahadharisha dhidi ya kuundwa taifa la muda la Wapalestina litakalokuwa na mipaka ya muda.

Rais Mahmoud Abbas pia amesema juhudi mpya zimeanzishwa kujaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na chama cha Hamas ingawa hatua kubwa haijapigwa.

Rais Mahmoud Abbas amerejea tena kauli yake kwamba atalazimika kuitisha uchaguzi mpya iwapo chama cha Hamas hakitaridhia mpango wa ushirikiano.

Rais huyo wa Palestina, alisema serikali yoyote ya umoja wa kitaifa ni lazima itimize masharti yatakayoiwezesha kuondolewa vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya magharibi dhidi ya serikali ya Hamas.

Marekani imekuwa ikishinikizwa na washirika wake kutoka Ulaya na pia mataifa ya Kiarabu kufufua mashauriano ya amani ya Mashariki ya Kati.