1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Wapalestina wajadili kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMA

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amekuwa na mazungumzo ambayo hayakukamilika juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na waziri mkuu Ismail Haniyeh mjini Gaza.

Chama tawala cha Haniyeh cha Hamas na kile cha Fatah kinachoongozwa na Abbas vimetia saini maikubaliano ya kugawana madaraka mwezi uliopita nchini Saudi Arabia.

Makubaliano hayo yalisitisha mapigano baina ya makundi hayo, lakini yalishindwa kufikia masharti ya mataifa ya magharibi na kuweza kuondoa vikwazo vya misaada ya kifedha hali inayodhoofisha utawala huo. Maafisa waandamizi wa Kipalestina wanasema kuwa mazungumzo ya hivi sasa yatachukua siku kadha , na kwamba kuna kutokuelewana kuhusuana na masuala kadha yahusuyo nafasi muhimu za baraza la mawaziri.

Kipindi cha wiki tano cha majadiliano kinamalizika March 21.