1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Tawi la kijeshi la Hamas limepigwa marufuku

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqp

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina ameiapisha serikali mpya ya dharura katika sherehe iliyofanywa kwenye makao yake makuu mjini Ramallah,katika Ukingo wa Magharibi.Muda mfupi baadae akalipiga marufuku tawi la kijeshi la chama cha Hamas.Katika baraza jipya la mawaziri, hakuna alie mwanachama wa Hamas,kinachofuata itakadi kali za Kiislamu.Rais Mahmoud Abbas wa Fatah,aliunda serikali mpya ya dharura,baada ya wanamgambo wa Hamas kuudhibiti Ukanda wa Gaza, kufuatia mapigano makali ya siku kadhaa.Ismail Haniyeh wa Hamas aliekuwa waziri mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa,ameipinga hatua ya Abbas ya kumfukuza kazi.

Waziri Mkuu mpya,Salam Fayyad ni mwanasiasa huru asie na chama,ni mchumi aliewahi kufanyia kazi Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki Kuu ya Dunia.Chama cha Hamas,kimesema serikali mpya iliyoapishwa hii leo si halali.