RAMALLAH : Rais wa Palestina huenda akaitisha uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH : Rais wa Palestina huenda akaitisha uchaguzi

Wasaidizi wa Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wamesema kiongozi huyo anatarajiwa kutangaza uchaguzi wa mapema katika hotuba yake muhimu mwishoni mwa juma lijalo.

Hali hiyo inakuja baada ya Abbas kusema kwamba haoni faida kuendelea na mazungumzo yaliokwama na serikali inayoongozwa na Hamas juu ya uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh akiwa zirani nchini Iran ameonya kwamba uchaguzi wa mapema utakuja kusababisha machafuko zaidi kwa Wapalestina.Pia amemshutumu Abbas kwa kujaribu kuwaondowa kwa nguvu mawaziri wa Hamas katika nyadhifa muhimu za serikali.

Serikali ya Hamas imegoma kusalimu amri kwa madai ya mataifa ya magharibi ya kukanusha matumizi ya nguvu na kuitambuwa Israel jambo ambalo limepelekea Marekani na Umoja wa Ulaya kusitisha misaada ya kifedha kwa Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com