RAMALLAH : Abbas ataka kikosi cha kimataifa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 10.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH : Abbas ataka kikosi cha kimataifa Gaza

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi leo hii amerudia tena ombi lake la kuwekwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani katika Ukanda wa Gaza.

Pendekezo hilo kwa kiasi kikubwa linaonekana kuwa haliwezi kutekelezeka kwa sababu ya matatizo mengi sana ya kutuma vikosi kwenye eneo tata kama hilo.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Prodi amedokeza kwamba wakati sio muafaka kwa jambo hilo. Msemaji wa kundi la Hamas lanalodhibiti Ukanda wa Gaza amesema kundi lake halitokubali uwekaji wa kikosi hicho ambacho watakihesabu kuwa kikosi cha mabavu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com