1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Wulff akiri makosa lakini hatajiuzulu

5 Januari 2012

Rais wa Ujerumani Christian Wulff amesema simu ya hasira aliopiga kwa Mhariri Mkuu wa gazeti maarufu la Bild, lilikuwa kosa kubwa lakini amesisitiza kwamba hana makusudi ya kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/13eYu
Bundespräsident Christian Wulff begrüßt Bürger der Stadt am Donnerstag (17.03.2011) in Osnabrück. Der in Osnabrück geborene Politiker besucht an diesem Tag auch das neue Volkswagenwerk Osnabrück (ehemals Karmann) zum Produktionsstart des neuen Golf Cabrio. Foto: Friso Gentsch dpa/lni
Rais wa Ujerumani Christian Wulff akisalimiana na watuPicha: picture-alliance/dpa

Rais Wulff aliyasema hayo jana katika mahojiano na Televisheni ya serikali.

Rais Wulff alipiga simu hiyo wakati gazeti la Bild lilipokuwa linatayarisha kuchapisha habari juu ya mkopo ambao aliupata ili kununua nyumba kwa ajili ya familia yake.

Rais Wulff alisema katika mahojiano ya dakika 20 kuwa anajua hakufanya chochote kinyume na sheria, lakini pia alieleza ,kwamba siyo kila alichokifanya kilikuwa sahihi.

Rais Wullf ameomba radhi juu ya simu aliyoipiga kwa gazeti la Bild.

Gazeti hilo liliripoti kwa mara ya kwanza tarehe 13 mwezi Desemba kwamba Rais Wulff aliupokea mkopo binafsi wa Euro lakini tano kutoka kwa

mke wa mfanyabiashara mmoja.

Bwana Wulff alipewa mkopo huo alipokuwa Waziri Mkuu wa jimbo la Lower Saxony la kaskazini magharibi mwa Ujerumani.

Wabunge wa vyama vya upinzani katika jimbo hilo waliuliza iwapo bwana Wulff alikuwa na uhusiano wa kibiashara na rafiki yake wa miaka mingi Egon Geerkens.

Bwana Wulff alijibu kwa kusema kwamba hakuwa na uhusiano huo lakini hakutoa taarifa juu ya mkopo aliopewa.

Hata hivyo maafisa wa idara ya sheria wamesema hawaoni iwapo pana ushahidi wowote juu ya kutendeka kosa la jinai kuhusu mkopo huo.

Naibu wa Msemaji wa serikali ya Ujerumani aliwaambia waandishi wa habari kwamba Kansela wa Ujerumani Bibi Merkel anaithamini sana kazi ya Rais Wulff na msimamo huo haujabadilika.