1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa Peru Fujimori korokoroni

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNF

Lima:

Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori amerejeshwa nyumbani akitokea Chile,na kutiwa moja kwa moja korokoroni.Fujimori ,mwenye umri wa miaka 69 anatuhumiwa kuhusika na rushwa na kuvunja haki za binaadam alipokua madarakani kati ya mwaka 1990 hadi 2000.Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 30 jela pindi akikutikana na hatia.Bwana huyo mwenye asili ya Japan,aliamua kujiuzulu kama rais, miaka sabaa iliyopita alipokua ziarani barani Asia.Alikimbilia Japan. Alikamatwa mwaka 2005 alipotaka kuitembelea Chile.Mahakama kuu ya Chile iliamua ijumaa iliyopita Fujimori arejeshwe nchini Peru.