1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy aadhimisha miaka miwili tangu ainge madarakani.

6 Mei 2009

Ufaransa bado yakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.

https://p.dw.com/p/Hkdf
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.Picha: picture-alliance/abaca

Huku rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, akiadhimisha miaka miwili madarakani hii leo, watu wengi nchini ufaransa wanasema rais Sarkozy anafanya kazi mbaya, mifumo yake yake ni mibovu, huku uchumi ukiyumba.

Rais Sakozy hana cha kusherehekea. Ufaransa inakabiliwa na tatizo la ukosefu mkubwa wa ajira, huku naye rais Nicolas Sarkozy akikabiliwa na maandamano ya kupinga kila uamuzi anaoufanya

Lakini hata kama kura za maoni zinaonyesha umaarufu wake kukwama, chama chake cha UMP bado huenda kikaibuka mshindi kwenye uchaguzi wa bunge la ulaya mwezi ujao na pia kura ya maoni inaonyesha kuwa rais Sarkozy ana nafasi nzuri ya kuchaguliwa tena kama rais katika awamu ya pili baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha kwanza mwaka 2012.

Rais Sarkozy aliingia madarakani mwaka 2007 na kutoa ahadi za kuifanyia mabadiliko Ufaransa ambayo miundo mbinu yake iliyopuuzwa kwa muda mrefu imerudisha nyuma maendeleo.

Rais Sarkozy alileta sheria bungeni , akaifanyia mabadiliko sheria kuhusu kodi, akafanya mabadiliko kwenye taasi za elimu yaliyokuwa na matokeo mabaya, na pia kuondoa mfumo wa kufanya kazi masaa 35 kwa wiki ulioanzishwa na utawala wa kisoshalisti.

1. Mai in Frankreich Paris
Maandamano ya kumpinga ras Nicolas Sarkozy katika mji wa Paris nchini Ufaransa.Picha: AP

Lakini, hata hivyo, mabadiliko hayo yamekosa mwongozo na huenda rais Sarkozy akakabiliwa na hali iliyompta mtangulizi wake, Jacques Chirac, ambaye aliondoka madarakani na kuiacha ufaransa ikiyumba baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka kumi na mbili.

Taasisi ya Thomas More ambayo ni jopo la wataalamu huru jana jumanne lilitoa matokeo yake kulingana na kazi aliyoifanya Rais Sarkozy ambapo lilimpa alama 10.5 kati ya alama 20.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa rais Sarkozy ni lazima ajizatiti zaidi na kuitizama kwa undani mifumo yake ya uongozi na kuhakikisha kuwa ufaransa inajikwamua kutoka kwenye mgogoro wa kiuuchumi unaoikumba dunia.

Hata kama serikali ya ufaransa imeaza kutekeleza kati ya asilimai 77 ya ahadi alizotoa Sarkozy ni asilimia 40 tu ya ahadi hizo zilizotimizwa.

Mzozo wa kiuchumi umemwongezea matatizo zaidi rais Sarkozy, huku idadi ya wakosa ajira ikipanda kutoka asilimia 7.8 mwaka uliopita hadi asilimia 10 mwaka huu.

Mwandishi: Jason Nyakundi/RTR

Mhariri: Othman Miraji