1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran Ahmadinejad na Kambi ya Magharibi

15 Juni 2009

matokeo ya uchaguzi Iran ni ya kutatanisha- magharibi itabidi kuzungumza na Ahmadinedjad.

https://p.dw.com/p/IAFw

Kwa muujibu wa taarifa za habari,Kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Khemenei,amependekeza kuchunguzwa upya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Iran ambamo Ahmadinejad alitangazwa tayari mshindi.Ahamdinejad kwa jicho la sura ya mambo ilivyo nchini alivunja safari yake ya Urusi alao kwa sasa.

Wafuasi wa mpinzani wake Mousavi,wamekuwa wakilalamika majiani kupinga matokeo ya Tume ya Uchaguzi ya Iran.

Licha ya hali ya kutatanisha, yadhihirika kana kwamba, kambi ya magharibi haina budi isipokuwa kuendelea kuzungumza na Rais Ahmadinejad ambae hakupinga mkondo mpya wa mazungumzo na kambi ya magharibi.

Mhariri mmoja wa Israel aliyaeleza matokeo ya uchaguzi wa Iran ,kimsingi si mabaya hivyo kwa siasa za Israel.na laiti rais george Bush angelikuwa madarakani, angeridhika na matokeo hayo.Kwani, yakisaidia kuibakisha sura ya uhasama dhidi ya Iran.ingelitokea vyengine, mfuasi wa Bush,madarakani,Rais Barack Obama ,alifanya barabara kujizuwia kuingilia kati katika uchaguzi wa Iran na kutompendelea mtetezi mmojawapo.Kwani, ikitazamiwa kuwa Ahamadinejad angechaguliwa tena .

Ahmadinejad akimpotoa mno mpinzani wake na kumsema anatumikia maslahi ya nchi za nje na kutoa sifa kama hiyo,hakwendi sambamba na heba ya kutetea mapinduzi ya Iran...

Rais Ahamdinejad,licha ya kukaripiwa na wapżinzani ana azma ya kuzungumza na nchi za nje na hasa Marekani.Ingawa sio juu ya mada mradi wake wa nuklia,haki za binadamu,haki za wanawake au mgogoro wa mashariki ya Kati-mada za kawaida za kambi ya magharibi inapohusika Iran.

Rais Ahamdinejad anataka kumeleza rais Obama ,vipi ulimwengu mpya na uliobora unavyofaa kuwa.Ulimwengu ambamo si mataifa machache yana usemi ,bali umma wa dunia hii.

Kutoa sura kama hiyo ni jambo linalompendeza ,lakini rais Obama hatavutiwa na sura hiyo.Hatahivyo, rais wa marekani na washirika wake wakubwa wa kambi ya magharibi wakijua zamani kuwa dai lao walilotoa hadi sasa kuitaka Iran isimam ishe kurutubisha madini yake ya uranium,hawawezi kuilazimisha Iran kuliitikia.

Hata angelikuwa rais mwengine aliechaguliwa ,hali ingelikuwa sa hiyo.Ingawa si rasmi, wameshaanza kuiangalia Iran ni dola la kinuklia.Na hata nchini Israel kumekuwapo uchunguzi wa maoni ambao umeonesha winmgi wa waisrael wameshaungama Iran haizuwiliki kuwa ni dola la kinuklia.Juu ya hivyo, mazungumzo na Teheran hayatapungua umuhimu.

Mnamo miaka 30 iliopita, mizozano mingi ilirundikana kati ya Iran na Marekani kuwa sasa miaka 4 mengine kwa rais huyu huyu ,licha ya kuwa matokeo ya kuchaguliwa kwake bado yatatanishaa, hazingeweza kusubiri kuyapatia ufumbuzi.

Na msingi wa mazungumzo ya pande mbili sasa upo: Kwani, Iran haitaki kuamrishwa la kufanya na ni tabia hii ambayo pia Obama haipendi.

Kwamba, ingawa kimya kimya, Washington ikitazamia kiongozi bora wa kuzungumza nae kuliko huyu wa sasa ni dhahiri.Lakini, mtu hawezi kujichagulia adui wa kutatua matatizo yake.

Wairani na sio miongoni mwa wale tu waliovunjika moyo na matokeo ya uchaguzi, watakaribisha jinsi mazungumzo yatavyoendelea.Hwangependelea matumizi ya nguvu na fujo.Kwani, hayo huongoza katika maafa na mateso.

Ndio maana yafaa sasa kusubiri kuona ni hatua gani katika sera za ndani ya Iran, rais Ahmadinejad atachukua .