1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ghana asisitiza uwekezaji zaidi barani Afrika

Sekione Kitojo
1 Machi 2018

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ameanza ziara nchini  Ujerumani Jumatano, akidokeza kwamba msaada kutoka mataifa ya kigeni haujasaidia hadi sasa maendeleo nchini Ghana na kwamba umma katika baadhi ya sehemu ukwishazowea.

https://p.dw.com/p/2tUpe
Berlin, Ghanas Präsident Addo Dankwa bei Kanzlerin Merkel
Picha: picture-alliance/dpa/B.von Jutrczenka

Amesisitiza  kwamba mpango  hivi  sasa  ni  kuelekeza  nguvu  katika  biashara na  uwekezaji, kwa  lengo la  kuifanya Ghana  kugharamia  maendeleo yake  yenyewe.

Uhusiano  kati  ya  Ghana na  Ujerumani  hauko  katika  hali  mbaya. Ghana  inajikuta  katika  nafasi  ya mfano  kwa  mataifa  ya  Afrika magharibi, amepigia  upatu  Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel . Viongozi hao wawili Merkel na Akufo Addo wanataka  kuuimarisha  zaidi ushirikiano  uliopo  katika  suala  la  uchumi.

Ghanas Präsident Nana Akufo-Addo
Rais wa Ghana Nana Akufo-AddoPicha: picture alliance/dpa/AP Photo/G. V. Wijngaert

 Ujerumani inafanya  biashara  na  Ghana inayofikia kiwango  cha  euro milioni  584 kwa  mwaka  na  kuifanya  nchi  hiyo  kuwa  mshirika muhimu  wa  Ujerumani  katika  bara  la  Afrika, licha  ya  kuwa ikilinganishwa  na  biashara  na  mataifa  mengine  duniani , Ghana  iko nyuma sana. Akufo Addo alisema.

Uhusiano  wetu  na  Ujerumani  pamoja  na  mataifa  mengine yanayoendelea  unapaswa  kulenga katika  biashara  na  uwekezaji na sio  katika  kutoa  misaada. Enzi  za  kutoa  misaada  ya  maendeleo ilileta  hali  ya  utegemezi ,  ambayo  haikuweza  kuisaidia  Ghana hususan  katika  kufanya kazi  kwa  pamoja  katika  kile  kinachojulikana kama  mpango  wa "Compact with Afrika"  ikiwa  na  maana  Pamoja  na Afrika.

Mataifa  hayo  mawili  yanataka  kujenga  dhana  hiyo  kwa  pamoja. Juhudi  hizo  zinataka  kuingizwa  kwa  uwekezaji  zaidi  wa  makampuni binafsi  katika  Afrika.  Ujerumani mwaka  uliopita wakati  ikiwa  rais  wa kundi  la  mataifa yaliyoendelea  kiviwanda  na  yale  yanayoendelea G20 ilianzisha  juhudi  hizo. Kansela  wa  Ujerumani  amemwambia rais Akufo-Addo katika  mazungumzo  yao  kwamba , "tunapaswa  kuweka nguvu  zetu  zaidi ili uwekezaji  wa  makampuni  binafsi  kutoka Ujerumani  kwenda  Ghana  ufanikiwe  zaidi".

Deutschland G20 Afrika Treffen
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa pamoja na viongozi wa AfrikaPicha: Getty Images/AFP/J. Macdougall

Mpango wa "Pamoja na Afrika"

Merkel  amesema  kwamba  anatayarisha  mkutano  utakaofanyika  hivi karibuni  mjini  Berlin, utakaozihusisha  nchi  wanachama  wa  mpango huo  wa  Compact ili  kuangalia  yale  yaliyofikiwa.

"Waziri wa fedha wa Ghana anajishughulisha wakati  huu na  kufanikisha mpango  huo wa Compact, kwa kufanya mabadiliko nchini Ghana. Na kwa upande wetu hapa Ujerumani tunataka kusaidia uwekezaji binafsi ambapo hadi sasa haujakuwa wa kutosha  kwenda  Ghana ili kuweza kutekeleza mpango  huo".

Deutschland Stefan Liebing
Stefan Liebing mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa Ujerumani kuhusu AfrikaPicha: Afrika-Verein der deutschen Wirtschaft e.V.

Hadi  sasa  hata  hivyo  mpango  huo  wa  "Pamoja  na  Afrika" kwa mtazamo  wa  kiuchumi  haujaonesha  mafanikio.  Sera  ya  Ujerumani kuhusu  Afrika  inapaswa kuichukulia juhudi  hii  ya  pamoja  Afrika  kwa undani  zaidi, amedai  mwenyekiti  wa chama  cha  Afrika  katika  uchumi wa  Ujerumani , Stefan Liebing, kabla  ya  mkutano  baina  ya  Kansela Merkel na  Akufo-Addo.

Wenye  viwanda  nchini  Ujerumani, pamoja  na  halmashauri  ya biashara ,wameikosoa  serikali  kwa  kusema  hadi sasa  bado  hakuna uhakika unaotolewa  na  serikali  kwa  wafanyabiasha wa  Ujerumani, ambao  wanataka  kufanya  biashara  katika  bara  la  Afrika.

Suala  hilo  liliwasilishwa  kwa serikali  katika  miaka  ya  nyuma, suala ambalo  kutokana  na kampeni  za  uchaguzi  na  kipindi  kirefu cha ujenzi  wa  serikali  limewekwa  kando. Hata  serikali  ya  Ghana  bado inakazi  kubwa  ya  kufanya. Hususan  kukatikati  kwa  umeme, lakini pia masuala  ya  ufisadi pamoja  na hali  mbaya  ya  elimu, hali inayowatisha  wengi  wa  wawekezaji  wa  nje.

Verarbeitung von Kakaobohnen in Ghana
Zao maarufu wa kakao nchini GhanaPicha: dpa - Bildarchiv

Katika  mkutano  wao Merkel  na  Akufo-Addo wamekubaliana kufanyakazi  kwa  pamoja  katika  kupambana  na  uhamiaji  haramu. Vijana  hawapaswi  kupoteza  nguvu  zao  katika  jangwa  la  Sahara ama  katika  bahari  ya  Mediterania, badala  yake watumie nguvu  hizo kuijenga  upya Ghana, amesema  Akufo-Addo. Ujerumani inataka haraka warejeshwe  nyumbani  raia  wa  Ghana  ambao  waliomba  hifadhi nchini  Ujerumani  na  wakakataliwa. Kiasi  ya  Waghana 4,000 wanaishi  hivi  sasa  nchini  Ujerumani.

Mwandishi: Pelz, Daniel / ZR/ Sekione  Kitojo

Mhariri : Caro Robi