1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Chad atangaza hali ya hatari

15 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D7o0

NDJAMENA:

Rais wa Chad Idriss Deby ametangaza hali ya hatari kote nchini kuanzia usiku wa manane wa Februari 15 na amri hiyo itabakia kwa kipindi cha siku 15.Kuambatana na amri hiyo,watu hawana ruhusu ya kutoka majumbani mwao wakati wa usiku. Amri hiyo pia inaruhusu kusaka nyumba na kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari. Rais Deby amesema,udhibiti imara unahitajiwa ili kuweza kurejesha hali ya utulivu, kufuatia mashambulizi ya waasi katika mji mkuu Ndjamena,mapema mwezi huu. Deby amemtuhumu rais wa nchi jirani Sudan,Omar al-Bashir kuwa ametoa msaada kwa waasi hao.Sudan lakini mara kwa mara imekanusha tuhuma hizo.