1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Sarkozy awaasa viongozi wa Lebanon kuzingatia makubaliano

7 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EFIo

BEIRUT

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufarsansa amewatolea mwito viongozi wa Lebanon kuzingatia maridhiano kupitia mazungumzo na kujitolea katika makubaliano yaliyofikiwa ambayo yalituliza ghasia zilizokaribia kuitumbukiza tena nchi hiyo kwenye vita vya wenywe kwa wenyewe.

Sarkozy ambaye anaongoza ujumbe mzito katika ziara ya siku moja nchini humo ni kiongozi wa kwanza wa nchi za magharibi kutembelea Lebanon tangu kuchaguliwa Michel Suleiman kuwa rais mwezi ulopita.

Mazungumzo ya amani ya nchi hiyo yalisimamiwa na wapatanishi wa Qatar na kufikiwa makubaliano mjini Doha baada ya kutokea vurugu mbaya kabisa nchini Leabon ambazo hazijawahi kushuhudiwa tangu vita vya mwaka 1975 hadi mwaka 1990. Mkuu wa majeshi Michel Suleiman alichaguliwa rais chini ya makubaliano hayo ya Qatar lakini viongozi wamekuwa wakiendelea kuvutana bado juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Sarkozy amezungumza na Suleiman kabla ya kukutana katika dhifa ya mchana kwenye makao ya rais ambayo itahudhuriwa na viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa nchini Lebanon ikiwa ni pamoja na chama cha Hezbollah.