1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Medvedev asema juhudi zitaendelea Mashariki ya Kati.

Abdu Said Mtullya23 Juni 2009

Rais Dmitry Medvedev wa Urusi aanza ziara barani Afrika.

https://p.dw.com/p/IXkr
Rais Dmitry Medvedev wa Urusi alieanza ziara barani Afrika leo.Picha: picture-alliance/ dpa


Rais Dmitry Medvedev wa Urusi amesema mchakato  wa kufufua  juhudi za kuleta  amani  ni mgumu katika Mashariki ya Kati  lakini  ameahidi kuwa nchi  yake itaendelea na juhudi hizo  hadi mafanikio  yapatikane.

Rais Medvedev  amesema  hayo leo mjini Cairo baada ya mazungumzo  yake na  rais Hosni Mubarak wa Misri.

Misri ni kituo  cha kwanza katika  ziara yake barani  Afrika.

Rais  Medvedev aliwaambia   waandishi habari baada  ya mazungumzo yake na mwenyeji  wake  rais Hosni Mubarak  wa Misri kwamba suala  la  Mashariki ya Kati  ni gumu sana  lakini amesema licha ya  hayo Urusi ipo tayari kuendelea na juhudi   za ,kutafuta  ufumbuzi. 

Kwa upande wake rais Hosni Mubarak amesisitiza umuhimu wa Urusi katika juhudi hizo lakini amesema kuwa ufumbuzi hautapatikana  kutokana na juhudi za nchi moja tu.

Urusi na Misri  zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa muda mrefu.

Rais Medvedev na mwenyeji wake rais Hosni Mubarak wa Misri pia wamejadili njia  za  kuimarisha uhusiano katika baina ya nchi  zao  katika sekta za uchumi  na  biashara.

Kwa mara ya mwisho  ziara ya rais  wa Urusi  barani Afrika ilifanyika miaka mitatu iliyopita.

Rais Medvedev anafanya ziara  barani Afrika  muda mfupi  baada  ya rais Barack  Obama wa  Marekani  kutoa hotua yake  ya kihistoria mjini Cairo hivi karibuni,  ambapo alijaribu kuweka msingi  wa  uhusiano mpya na nchi  za kiislamu.

Baada ya  ziara  ya  nchini  Misri  rais Dmitry  Medvedev  pia  atazitembelea Nigeria, Namibia  na Angola kuanzia kesho.


Mwandishi:A.Mtullya/AFPE

Mhariri:AbdulRahman