1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kikwete ziarani nchini Marekani

20 Mei 2009

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo ataonana na Rais Barack Obama wa Marekani mjini Washington.

https://p.dw.com/p/HuDv
Rais Barack Obama kukutana na Rais Jakaya KikwetePicha: AP

Tanzania ni mshirika imara wa Marekani katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara na itakuwa ziara ya kwanza ya kiongozi wa kiafrika katika Ikulu ya Marekani tangu Obama ashike rasmi wadhifa wa Urais Januari mwaka huu.

Mohamed Abdulrahman alizungumza na Profesa Frank Chiteji akiwa Marekani na kwanza alimuuliza ziara hii ina umuhimu gani na anafikiri ni masuala gani yatakayopewa kipa umbele.

Mwandishi: Mohamed Abdulrahman

Mhariri: Thelma Mwadzaya