1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Köhler wa Ujerumani ziarani nchini Algeria

12 Novemba 2007

Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Ujerumani, Horst Köhler, alitangaza kwamba masuala ya Afrika yatakuwa ni mada muhimu katika kipindi cha wadhifa wake. Hivi sasa, rais huyo, kwa mara ya nne yuko katika ziara ya siku kadhaa barani Afrika ili kujijulisha juu ya mafanikio yaliopatikana na matatizo yalioko.

https://p.dw.com/p/CH72
Rais Horst Köhler wa Ujerumani akiwa katika meza yake ya kazini.
Rais Horst Köhler wa Ujerumani akiwa katika meza yake ya kazini.Picha: AP

Kituo cha mwanzo cha ziara yake ni mji mkuu wa Algeria, Algiers, ambako huko ameufungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la Ushirika na Afrika. Katika kongamano hilo wanashiriki wawakilishi wa nchi za Kiafrika, wale wa kundi la nchi nane zinazoongoza kiviwanda duniani pamoja na wale wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo,OECD.

Kuwa pamoja, na kila mmoja kujifunza kutoka kwa mwengine ili kuweza kutenda kwa pamoja. Hiyo ndio kauli mbiyu iliotolewa na Rais wa Ujerumani , Host Köhler, katika ufunguzi wa Jukwaa la Ushirikiano na Afrika.

+Binadamu anaishi katika jamii yenye mustakbali wa kutegemeana, na lazima tujitahidi tubebe dhamana kwa pamoja na tujifunze kwa pamoja.+

Mbele ya wawakilishi wa kundi la nchi nane zinazoongoza kiviwanda duniani, wa nchi za Kiafrika na wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OECD- jumuiya ya nchi fadhili, Rais Köhler alitoa mwito wa haraka wa kutolewa misaada zaidi kwa watu kuweza baadae wajisaidie wenyewe. Alisema kuweko masharti ya haki katika biashara pamoja na kuondoshwa vizuwizi vya forodha kwa ajili ya mazao yanayotokea barani Afrika ni jambo linalohitaji kufanywa kwa haraka. Rais Köhler alitoa mwito wa kuzidishwa majadiliano juu ya ya haja ya kuweko demokrasia na dola kuendeshwa kwa njia za sheria. Alisema Afrika ina matatizo ambayo lazima yenyewe iyatanzuwe.

+ Mara nyingi kuna uongozi mbaya wa serekali, au, kwa mfano, ule ukweli kwamba Waafrika wenyewe ule uwezekano wa kubadilishana ndani ya Afrika yenyewe, kushirikiana na kufungamana wanautumia kwa uchache sana.+

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani, Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul, bembezoni mwa jukwa hilo, alisisitiza juu ya kutegemeana baina ya Ulaya na Afrika. Ushirikiano zaidi wa kifedha na Afrika ndio mtizamo wa Ujerumani.

…ubwa kwamba katika eneo la Afrika kuna utulivu, utulivu ambao ni shuruti ya kuweko utulivu wa kijamii. Na ni muhimu kwamba watu wenyewe wafaidike na wahisi kwamba hali zao za maisha zinaboreka.+

Kwa tabaka kubwa ya wananchi wa Algeria, licha ya mapato makubwa ya nchi hiyo kutokana na gesi ya ardhini na mafuta, hali zao sio nzuri. Hasa ukosefu wa nafasi za kazi miongoni mwa vijana ni mkubwa sana.Jana Rais wa Ujerumani alizungumzia hasa mada hiyo jana alipokutana na wasomi wa nchi hiyo. Mtizamo wake:

+Tunahitaji siasa na mwenendo unaoweza kuchunguzwa ambao utahakikisha kwamba utajiri wa mali za asili za Afrika unawafaidia watu wote wa Afrika.+

Hivyo hasa vijana wa Algeria lazima waingizwe katika mazungumzo juu ya mustakbali wa nchi yao. Rais wa Ujerumani na waziri wa maendeleo wanakubaliana katika jambo hilo. Hasa vijana wa Algeria hawafahamu kwanini wanatengwa. Hawapati visa za kwenda nje kufanya utalii. Waziri Wieczorek-Zeul alisema hilo ni tataizo la Ulaya:

Insert: O Ton …

+Sisi, Ulaya na Afrika, kwa hakika, tumetengana kwa kilomita 12. Ndio maana ninajaribu kila wakati kusisitiza kwamba sisi lazima tuboreshe hali za maisha ya watu katika Afrika. Hivyo kutotawala ile fikra ya kutaka kuhama na kutoka nje ya nchi na kutaka kutafuta maisha mazuri ya Ulaya.+

Jukwa hil la tisa la Ushirika na Afrika pia litazungumzia juu ya Uchina. Nchi hiyo kubwa yenye uchu wa nishati zamani imeshtambua nafasi ilio nayo katika Afrika na inashirikiana na nchi za Kiafrika, licha ya kukiuka vipimo vya nchi za magharibi juu ya demokrasia na haki za binadamu, jambo linalowaudhi watu wengi wa Ulaya.