1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Horst Köhler wa Ujerumani aahidi kusaidia demokrasia nchini Mauritania

15 Novemba 2007

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesema nchi yake inadhamiria kusaidia juhudi za Mauritania katika kupambana na umasikini.

https://p.dw.com/p/CH6r
Rais Wa Ujerumani Horst Köhler
Rais Wa Ujerumani Horst KöhlerPicha: picture-alliance/ dpa

Rais Köhler amesema hayo katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Mauritania.Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema hayo baada ya mazungumzo na wenyeji wake mjini Nouakchott.

Amesema Ujerumani inadhamiria kushirikiana na Mauritania katika juhudi zake za kujenga demokrasia na kupambana na umasikini.

Rais Köhler amesema anafanya ziara nchini Mauritania ili kuendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya Ujerumani na nchi hiyo.Ameeleza kuwa Mauritania sasa ipo katika kipindi ambapo demokrasia inajengeka na kwamba nchi hiyo inahitaji kuungwa mkono.

Ameahidi kuwa Ujerumani itashirikiana na watu wa Mauritania ili demokrasia isimame kwa miguu yote miwili nchini humo

AM.