1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Gauck ziarani Zanzibar

Elizabeth Shoo4 Februari 2015

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck amewasili Zanzibar kwa ziara ya muda mfupi. Gauck alipokewa kwenye bandari ya Zanzibar na Rais wa visiwa hivyo Dr Ali Mohammed Shein na umati mkubwa wa wananchi.

https://p.dw.com/p/1EVLB
Rais Gauck nchini Tanzania
Picha: DW / Khelef Mohammed

Ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita nchini Tanzania, Gauck huko Zanzibar anahudhuria pia kongamano la viongozi wa dini. Baada ya hapo, rais Gauck anaelekea mjini Arusha. Mohammed Abdul-Rahman amezungumza na mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar Salma Said kufahamu jinsi wananchi wa visiwa hivyo wanavyoiangalia ziara hiyo.

Kusikiliza mahojiano hayo, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Elizabeth Shoo

Mhariri: Josephat Charo