Rais Bush ziarani mashariki ya kati | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 09.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Rais Bush ziarani mashariki ya kati

---

WASHINGTON

Rais George Bush anaekelea Mashariki ya Kati leo hii katika ziara yake ya kwanza kwenye eneo hilo tangu alipochukuwa uongozi nchini Marekani.Rais Bush ataanzia ziara yake nchini Israel na Ukingo wa magharibi kujaribu kutia msukumo mazungumzo ya amani katika eneo hilo la mashariki ya kati mazungumzo ambayo yalifufuliwa mwezi Novemba mwaka jana mjini Annapolis.

Lengo la rais Bush katika ziara hiyo ni kuhakikisha anaweka mkakati wa kupatikana suluhu itakayoweza kusaidia kuundwa kwa dola la Palestina kabla ya kumalizika mwaka huu.Baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina Bush atazitembelea nchi tano za kiarabu ambazo ni washirika wake katika eneo hilo.Agenda yake kuu katika nchi hizo ni kuwakumbusha viongozi wa kiarabu kusaidia katika kupatikana suluhisho la mataifa mawili yatakayoishi bega kwa bega.

 • Tarehe 09.01.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CmmB
 • Tarehe 09.01.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CmmB

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com