1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush aukagua mwaka 2007

21 Desemba 2007

Rais George Bush wa Marekani katika mkutano na waadishi habari alikagua sera zake juu ya Iraq,Russia na Afghanistan.

https://p.dw.com/p/Ceep
Rais Bush wa MarekaniPicha: AP

Rais George Bush wa Marekani akiukagua mwaka huu wa 2008 madarakani ulivyokwenda, alijaribu jana kupunguza wasi wasi mkubwa uliopo juu ya sera zake nchini Iraq,Afghanistan na akaahidi kuikagua Russia kwa makini mwakao ujao wa 2008.

Ramadhan Ali na ripoti zaidi:

Rais Bush , katika kile kilichobainika mkutano wake wa mwisho na waandishi habari kwa mwaka huu wa 2007, alijaribu pia kuzima ghadhabu iliozuka juu ya tuhuma za mateso za majasusi wa shirika la Marekani la CIA kwa watuhuimiwa ugaidi.Alidai watu wengi wanapendelea kile Marekani inachotetea ulimwenguni.

Rais Bush anaeacha madaraka januari, 2009 alitoa changamoto hadharani alipohoji iwapo rais Wladmir Putin wa Russia atamuachia kweli waziri mkuu alieteuliwa Russia Dmitry Medvedev kudhibiti hatamu za uongozi wa nchi na akatilia shaka wazi wazi kujitolewa kidhati wa Russia kuleta mageuzi ya kidemokrasi.

Rais Bush akamtaka rais Putin anaetarajiwa baadae kushika wadhifa wa waziri-mkuu a asie na kigeugeu n a swali la kimsingi aliuliza Bush:kutokua na kigeugeu kuelekea shabaha gani ?

Je, unajua Russia itakuaje miaka 10 kutoka sasa ?- aliuliza George Bush.

„Matumaini yangu“, alisema Bush „ni kuwa Russia ni nchi inayotambua mahitaji ya kuwapo nchini vyombo vinavyoikagua serikali inayotenda,uchaguzi huru na wa haki.Russia inayoelewa desturi za nchi za magharibi zinazoegemea haki za binadamu na utu wake na ndizo desturi zitakazoiongoza kuwa nchi bora-alisema rais Bush.

Akasema kwamba atakua akiiangalia sasa Russia inapiga hatua gani na kungoja kuona iwapo rais Putin atakuja kuwa waziri mkuu,lakini atamkodolea macho kumuona jinsi anavyomuongoza rais wa Russia kuendesha shughuli zake.

Vita visivyopendwa nchini Iraq na hali ya wasi wasi katika usalama nchini Afghanistan vikitarajiwa kugubika kampeni ya uchaguzi wa Novemba mwaka ujao war ais wa marekani, rais Bush alielezea matumaini ingawa kwa hadhari kuwa hali itatengenea , lakini George Bush alisema tangu Iraq hata Afghanistan lazima zioneshe zinapiga hatua ya maendeleo.

„Swali ninalouliza kuhusu Iraq na Afghanistan ni hili:Je, kuna maendeleo yoyote yanayofanyika huko ? Je, wananchi wa huko wanahisi maisha yao sasa ni bora kuliko yalivyokua ? Akijibu alisema Bush , „Naamini tunafanya maendeleo pande zote mbili.“

Hatahivyo, George ush aliungama kuwa mpango wake wa mwaka mzima wa kuimarisha majeshi nchini Iraq ili kuzima machafuko haukuzaa matunda mema ya kurejesha suluhu na maelewano kitaifa.

George Bush alionesha hata kuvunjika zaidi moyo na hali nchini Afghanistan ambako mwaka huu wa 20007 ndio ulioshuhudia umwagaji mno damu tangu pale Marekani ilipoongoza majeshi ya washirika wake kuivamia nchi hiyo hapo 2001.Wanamgambo wa Taliban na Al-Qaeda walichachamaa mno mwaka huu na mavuno ya maua yanayotengezewa –opium-yalinona.

Akiungama kwamba baadhi ya washirika wake wa NATO wameanza kuonesha kuchoshwa na vita nchini Afghanistan, George Bush alitangaza na ninamnukulu:

„Wasi wasi wangu mkubwa ni kwa watu kusema tumechoshwa na balaa la Afghanistan na hivyo tuiache mkono.“

Akasaema itachukua muda kwa majaribio ya kidemokrasi nchini Afghanistan kufanya kazi na anaamini demokrasia itafanya kazi.

Akitupia macho wiki 3 zijazo kwa ziara yake ya kwanza nchini Israel na ukingo wa Magharibi, Bush alisema anatumai ameweza kuusogeza usoni „Utaratibu wa amani kati ya Israel na Palestina“ baada ya miaka mingi ya kutuhimiwa kuwa akidharau kufanya juhudi hizo.

Kuhusu badiliko la hali ya hewa, Rais George Bush alishikilia kudai anatia maanani sana tatizo hilo.