1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush ainyoshea kidole Syria

14 Juni 2007

Mbunge wa Lebanon alieuwawa jana katika hujuma ya bomu Walid Eido-mkosoaji wa siasa za Syria Lebanon, amezikwa leo.Tangu Iran,UM hata Umoja wa Ulaya zimelaani hujuma ya jana mjini Beirut.

https://p.dw.com/p/CHCg

Rais George Bush wa Marekani, ameinyoshea leo kidole Syria kuhusika na mripuko wa jana wa bomu mjini Beirut,Lebanon uliomuua mbunge wa anaeikosoa mno Syria- Walid Eido.Eido amezikwa hii leo.

Baraza la Usalama la UM na Iran –mshirika wa chanda na pete wa Syria, halkadhalika, limelaani shambulio hilo lililofanyika katika mwambao wa pwani wa Beirut hapo jana.Jumla ya watu 10 pamoja na mbunge huyo waliuwawa.

“Kumekuwapo na mtindo wazi kabisa wa kuua na kujaribu kua wanasiasa nchini Lebanon tangu oktoba,2004.”-alisema rais Bush kattika taarifa yake aliotoa juu ya mauaji ya jana.

Akaongeza kusema,

“wale wanaopigania Lebanon huru nay a kidemokrasia, daima ndio wanaolengwa kuuliwsa.Wahanga daima wamekuwa wale waliotaka kukomesha kujiingiza ndani ya mambo ya Lebanon kwa mkono wa rais Assad wa Syria.”

Rais Bush alisema zaidi kuwa Marekani itaendelea kuiungamkono Lebanon,watu wake na serikali yake halali ikikabili hujuma hizo.

Mbunge wa Lebanon Walid Eido aliezikwa hii leo ni mhanga mwengine katika msururu a mauaji ambayo serikali ya muungano inayotawala Lebanon imeilaumu Syria kuhusika.Katika maafa ya jana, hata motto wa kiume wa marehemu na walinzi wake 2 ni miongoni mwa waliouwawa.

Hali nchini Lebanon itakua mada hapo kesho katika kikao cha mawaziri wa nje wa Jumuiya ya nchi za kiarabu-Arab League .Kikao hicho kinaitikia ombi rasmi la waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora aliesema m auaji ya m bunge Eido ni sehemu ya njama ya kuiodhofisha na kuisambaratisha Lebanon.

Tangu kuuwawa kwa waziri-mkuu wa zamaniwa Lebanon, Rafiq Hariri,februari,2005,Syria,jirani wa Lebanon, imekuwa ikishinikizwa ulimwenguni.Mpinzani mwengine maarufu wa Syria-waziri Pierre Gemayel alipigwa risasi na kuuliwa Novemba mwaka uliopita.

Baraza la Usalama la Um ambalo Mei 30 liliidhinisha Mahkama ya kimataifa kusimamia kesi ya kuuwa kwa Hariri limesema linalaani kwa ukali kabisa shambulio la jana la kigaidi.Lilisema zaidi kuwa wanachama wa Baraza hilo wanalaani jaribio lolote la kuichafua Lebanon hata kwa njia ya mauaji ya wanasiasa wake au njia nyengine.

Iran,mshirika wa chanda na pete wa Syria ,imelaani pia shambulio hilo.

Mfalme Abdullah wa Jordan ameipelekea risala serikali ya Lebanon ndani yake akilaani kwa ukali kabisa shambulio la jana.

Ujerumani ikiwa rais wa sasa wa UU pia imesikitishwa na mripuko huo.

Syria imekanusha mafungamano yoyote na mauaji ya waziri mkuu Hariri na haikudhukuru bado lolote juu ya shambulio la jana.