1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush aikosoa China

7 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/EsHt

Rais George W Bush wa Marekani yumo njiani kuelekea China kuhudhuria shehere ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki hapo kesho. Ndege inayombeba rais Bush imeondoka mjini Bangkok baada ya kiongozi huyo kufanya ziara iliyodumu chini ya muda wa saa 24 nchini Thailand. Katika hotuba yake mjini Bangkok rais Bush amesifu kuenea kwa uhuru barani Asia lakini akaikosa vikali China, Myanmar na Korea Kaskazini kwa ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu.

Nchini Thailand, rais Bush pia alikitembelea kituo kinachojulikana kama Mercy Centre ambacho ni makaazi ya watoto 4,000. Kituo hicho kina hospitali na ni nyumbani kwa akina mana na watoto wanaoishi na maradhi ya ukimwi.

Mke wa rais Bush, Laura Bush, alikutana na wakimbizi ambao wamelengwa katika kampeni ya ukandamizaji inayofanywa na utawala wa kijeshi wa Myanmar. Akiandamana na mume katika ziara ya barani Asia, Laura alisafiri kwenda katika mpaka kati ya Thailand na Myanmar kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Mae La, ambako ni makao ya watu 38,000 wa kundi dogo la Karen ambalo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema linalengwa katika mauaji ya kiijeshi, ubakaji na kuchomea vijiji vyao.

Watu takriban 200 wamekamatwa katika eneo hilo la mpakani, wengi wao wanafunzi kutoak Myanmar waliotaka kukutana na rais Bush na mkewe Laura kuwaomba wasaidie kudumisha demokrasia nchini mwao.