1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assad Rede

Abdu Said Mtullya30 Machi 2011

Rais Al-Assad wa Syria adai kwamba upinzani dhidi yake unatokana na njama kutoka nje

https://p.dw.com/p/10kvD
Maalfu ya watu wakiwa katika maandamano nchini SyriaPicha: picture alliance/dpa

Rais Bashar Al-Assad wa Syria amesema leo katika hotuba yake kwamba upinzani unaofanyika dhidi ya utawala wake unatokana na njama Hayo anasema mwandishi wetu Rainer Sollich katika maoni yake yafuatayo:

Hotuba ya leo ilikuwa fursa kubwa kwa Rais Bashar Al-Assad. Angeliweza kuitumia fursa hiyo kuanzisha hatua muhimu za mageuzi ya kidemokrasia nchini wakati ambapo sasa anakabiliwa na upinzani. Pia angeliweza kujiimarisha kama kiongozi mwenye kipawa cha kuona mbali kisiasa.Lakini wala hakujaribu kufanya hayo.

Badala yake Rais Bashar Al-Assad alitumia mbinu za bei ya chini za propaganda. Amevilaumu vyombo vya habari vya nje kwa kusambaza habari za kupotosha kwa kudhamiria.

Ametoa hotuba yake mbele ya wabunge waliokuwa wanashangalia japo kila mtu anajua kwamba wabunge hao hawakuchaguliwa kwa njia huru. Na wala Rais huyo hakutahayari kuwapachika wabunge maalumu kwa ajili ya kumsifu. Njama hizo zinajulikana kwani zinafanywa na viongozi wa Korea ya Kaskazini.

Syria inahitaji mageuzi.Hakuna uhuru wa kutoa maoni katika nchi hiyo. Hakuna vyombo vya habari huru na wala hakuna upinzani.Rushwa imetanda kote nchini.Idara za ujasusi zinawadhibiti wananchi. Wapinzani wanasakiziwa makosa na kutiwa ndani.

Kwa mujibu wa habari watu zaidi ya 60 wameshauawa katika kipindi cha wiki mbili za maandamano ya upinzani dhidi ya utawala wa Al-Assad.Lakini hakuna anaeijua idadi ya uhakika ya waliouawa.

Rais huyo pia hakuwa na ujasiri wa kuondoa hali ya hatari kama ilivyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Leo ametoa hotuba isiyotoa matumaini juu ya mustakabali ambao kwa kweli hakuna anaeutegemea.Hotuba yake itawakasirisha zaidi wapinzani.

Na hata hatua ya baraza lake mawaziri kujiuzulu jana ilikuwa kazi bure kutokana na ukweli kwamba baraza hilo halikuwa na mamlaka yoyote ya kisiasa.

Hata hivyo haitakuwa sawa kupuuza kiwango anachoungwa mkono na watu wake. Rais Al-Assad siyo sawa na aliekuwa Rais wa Misri Mubarak.Al-Assad ni maarufu miongoni mwa watu wake hasa kutokana na msimamo wake thabiti dhidi ya Marekani na Israel.

Lakini vilio juu ya uhuru na demokrasia haviwezi kufunikizwa nchini Syria vile vile. Jinsi utawala wa Al- Assad utakavyojaribu kuvinyamazisha vilio hivyo inafahamika.Kuna uwezekano wa hali kuendelea kushatadi.

Mwandishi/Sollich Rainer/Dw-intern/

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mhariri/-Abdul-Rahman/