1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Saudia warudi nyumbani

29 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Chsl

DUBAI

Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imesema Raia 10 wa nchi hiyo waliokuwa wamezuiliwa katika jela ya Marekani ya Guantanamo Bay nchini Cuba wamerejea nyumbani hii leo.

Marekani imewarudisha ynumbani raia kadhaa wa Saudi Arabia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kama hatua ya kupunguza idadi ya wanaoshikiliwa katika kambi hiyo inayozua utata kabla haijafungwa.Hata hivyo kiasi cha raia 13 wa Saudia bado wanazuiliwa katika kituo hicho ingawa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo mwanamfalme Nayef Bin Abdul-Aziz amesema juhudi zinafanyika za kuwarudisha nyumbani wanaoendelea kushikiliwa.