1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Mali wapiga kura licha ya hofu ya kutokea Ghasia

Mjahida25 Novemba 2013

Raia wa Mali walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa bunge licha ya hofu kwamba uchaguzi huo ambao unaoonekana kuwa hatua ya mwisho ya kuwepo kwa utawala wa kikatiba huenda ukakumbwa na mashambulizi ya waasi.

https://p.dw.com/p/1ANZA
Raia wa Mali ashiriki katika uchaguzi, jana
Raia wa Mali ashiriki katika uchaguzi, janaPicha: Reuters

Nchi hiyo ya Mali ambayo inashuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi, tangu wanajeshi walioasi kufanya mapinduzi nchini humo mnamo Machi mwaka wa 2012.

Hatua hiyo ndiyo iliotoa nafasi kwa makundi mengine ya waasi kama Tuareg na wanamgambo waliona itikadi kali za kidini walio na mafungamano na kundi la Al Qaeda kuchukua udhibiti wa eneo zima la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Awali vikosi vya kijeshi vya Ufaransa viliingilia Mali kijeshi mwezi wa Januari, na kufanikiwa kuwafurusha waasi kutoka kwa baadhi ya maeneo waliokiuwa wameyadhibiti.

Hata hivyo ghasia zimezidi kuonekana nchini humo katika wiki za hivi maajuzi na kutoa changamoto kubwa ya kiusalama kwa rais Ibrahim Boubakar Keita.

Maafisa wa jeshi wakilinda usalama wakati wa uchaguzi
Maafisa wa jeshi wakilinda usalama wakati wa uchaguziPicha: picture-alliance/AP

Kulingana na Mohamed Ag Mossa mkaazi wa mji wa Kidal, watu watatu walijeruhiwa hapo jana baada ya wafuasi wa waasi wa kituaraeg kuwarushia mawe wapiga kura na kusababisha majeshi ya Kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Mjini Timbuktu masanduku 10 ya kupigia kura yaliibiwa na watu wasiojulikana kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama wa Mali. kumekuwa pia na matatizo ya usajili wa wapiga kura yalioripotiwa katika zoezi zima la uchaguzi.

"Sikuona picha yangu wala jina langu katika orodha ya wapiga kura nimesikitika sana kwa sababu sikuwa kupiga kura," Alisema Bintou Maiga mkaazi wa Timbuktu.

Idadi ndogo ya watu wajitokeza katika uchaguzi

Kwengineko wengi wa wapiga kura mjini Gao wamesema suala la usalama lilikuwa katika fikra zao, ndio maana ni idadi ndogo ya watu iliyojitokeza katika zoezi hilo ikilinganishwa na uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi wa Julai na Agosti wakati raia wa nchi hiyo walipomchagua Ibrahim Boubacar Keita kuwaongoza.

Wakati huo huo waasi wa Tuareg Kaskazini Mashariki mwa Mali wamezuia uchaguzi kufanyika katika eneo lao. Wafuasi wa kundi hilo walioandamana waliharibu masanduku ya kupigia kura huku wakisema kwa sauti kuwa hawataki uchaguzi wanataka uhuru.

Tangu alipochaguliwa rais Keita amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwaunganisha watu wote wa Mali, kuunda baraza jipya la mawaziri kushughilikia maendeleo ya Mali. Takriban watu milioni 6 na nusu walisajiliwa katika zoezi hilo la kuwachagua wabunge 147 kati ya wagombea 1000 walioshiriki.

waandishikishaji wa uchaguzi
waandishikishaji wa uchaguziPicha: picture-alliance/AP

Umoja wa Ulaya tayari una waangalizi wake wa kura zaidi ya 100 katika uchaguzi huo waliopelekwa katika vituo vyote nchini humo.

Huku hayo yakiarifiwa Mamouni Soumano, mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Mali amesema kutokana na idadi ndogo ya watu ilioshuhudiwa katika zoezi la kupiga kura huenda kukawa na duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika Disemba 15.

Mwandishi Amina Abubakar/AP

Mhariri Yusuf Saumu