1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Irak akamatwa nchini Ujerumani kwa kuhusika na mtandao wa Al-Qaida

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD48

Polisi nchini Ujerumani wamemkamata raia moja wa Irak ambae anatuhumiwa kupeleka kwenye Internet taarifa za mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida wa Osama bin Laden. Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 36 na ambaye anatambuliwa kwa jina la Ibrahim R., amekamatwa katika mji wa Osnabrueck magharibi mwa nchi. Anatuhumiwa kuwa alisaidia katika shughuli za kigaidi kwa kupeleka kwenye Internet taarifa za viongozi wa Al-Qaida kama vile, Osama bin Laden, Ayman al- Zawahri na Abu Musab al Zarqawi.

Anatarajiwa kusikilizwa na mahakama kesho.