1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Radio na magazeti yafungiwa Rwanda

Josephat Nyiro Charo29 Julai 2010

Serikali ya Rwanda imekuwa ikizongowa na lawama kwamba inakandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini

https://p.dw.com/p/OXWQ

Baraza kuu la habari nchini Rwanda limetoa orodha ya vyombo vya habari ambavyo vinaruhusiwa kufanya kazi nchini humu, na kutoa onyo kwa vile ambavyo haviko kwenye orodha hiyo kuwa endapo vitaendelea kufanya kazi, sheria itachukua mkondo wake. Miongoni mwa vyombo vya habari ambavyo vimejikuta nje ya orodha hiyo ni pamoja na magazeti matatu ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa muda ya Umuseso, Umuvugizi na Umurabyo, ambavyo wahariri wake ama wako jela, au wameikimbia nchi.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikikabiliwa na shutuma kutoka kwa watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari kuwa inaukandamiza uhuru wa kujieleza, shutuma ambazo serikali hiyo inazikanusha. Sauti ya Amerika ni miongoni mwa vituo vitatu vya radio ambavyo sasa havina ruhusa kurusha matangazo nchini Rwanda.

Daniel Gakuba ametutumia report ifuatayo kutoka Kigali.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Josephat Charo