1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pristina. Mabalozi kutathmini hali halisi ya Kosovo.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6Q

Mabalozi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wamejionea kwa mara ya kwanza hali katika jimbo linalotaka kujitenga la Kosovo. Wajumbe hao wanataka kuangalia uwezekano wa kuangalia hatua za kuleta uhuru, kama zilivyopendekezwa katika mpango ambao wanahitajika kuupigia kura hivi karibuni.

Wanabalozi hao kutoka mataifa 15 wanachama wa baraza hilo la usalama walikutana na ujumbe wa kulinda amani wa umoja wa mataifa , ambao umekuwa ukiongoza jimbo hilo la Kosovo ambalo lina wakaazi wengi wa asili ya Albania tangu mwishoni mwa vita vya mwaka 1998-1999.

Waalbania wa Kosovo pia kwa mara nyingine tena wameeleza suala lao la kutaka uhuru kutoka Serbia katika majadiliano na wajumbe hao.

Hapo mapema mjini Belgrade , mabalozi hao walizungumza na viongozi wa Serbia, ambao wanapingana na mpango huo wa umoja wa mataifa wa kutoa uhuru kwa jimbo hilo. Mabalozi hao wanataka kuangalia jinsi Waalbania watakavyoweza kuwalinda Waserb wachache katika jimbo hilo.