1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA: Jeshi la ukombozi la Kosovo ladai kuhusika na shambulio la bomu

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ8

Kundi linalojiita jeshi la ukombozi la Kosovo, Kosovo Liberation Army, limesema lilifanya shambulio la bomu lililoyaharibu magari matatu ya Umoja wa Mataifa.

Hakuna aliyejeruhiwa katika shambulio hilo la juzi Jumatatu, lakini limeongeza hali ya wasiwasi huku mazungumzo yakiendelea kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.

Kundi hilo la zamani la waasi lilipigana na vikosi vya Serbia katika miaka 1990. Katika taarifa yake kundi la Kosovo Liberation Army limesema shambulio hilo la bomu lilikuwa la kulipiza kisasi vifo vya waandamanaji wawili Walbania.

Waziri mkuu wa Kosovo, Agim Ceku, aliyewahi zamani kuwa kiongozi wa kundi hilo, alilaani shambulio hilo akilitaja kuwa kitendo kinachopinga juhudi za kufikia uhuru wa Kosovo.