1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

POTSDAM: Urusi yapinga pendekezo la hali ya baadaye ya Kosovo

Kwenye mkutano wa mawaziri wa mashauri ya kigeni wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani, G8, Urusi imekuwa na msimamo tofauti kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.

Waziri wa kigeni urusi, Sergei Lavrov, amekataa pendekezo la waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinemer, kuitaka Moscow ikome kupinga mipango ya Umoja wa Mataifa kuhusu hatima ya jimbo la Serbia la Kosovo.

Akizungumza kwenye mkutano huo wa mjini Potsdam, Sergei Lavrov, amesema hali ya baadaye ya Kosovo inatakiwa iamuliwe kupitia mazungumzo baina ya serikali ya Belgrade na serikali ya Pristina. Serbia, inayoungwa mkono na Urusi, inauopinga mpango uliopendekezwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa, Mahrtti Ahtasaari, unaotaka uhuru wa Kosovo usimamiwe na jumuiya ya kimatiafa.

Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zinauunga mkono mpango huo. Mkutano wa mjini Potsdam ulioandaa mkutano wa nchi za G8 utakaofanyika wiki ijayo mjini Heligendamm hapa Ujerumani, umetuwama pia juu ya mizozo nchini Afghanistan, Darfur, Irak na Mashariki ya Kati.

Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka Pakistan na Afghanistan wamehudhuria mkutano wa mjini Potsdam kama sehemu ya juhudi za Ujerumani kuzipatanisha nchi hizo.

Wakati huo huo, pande nne zinazoudhamini mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, zikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi, zimekutana mjini Berlin kujadili mchakato wa amani baina ya Israel na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com