1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi yakamata gari lenye silaha na picha za kampeni

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS9T

Polisi ya Kenya hapo jana imelibamba gari lenye nambari za serikali lililosheheni silaha na picha za kampeni za Rais Mwai Kibaki.

Naibu kamanda wa polisi wa polisi wa mkoa amesema wamegunduwa mapanga,upinde na mishale pamoja na viboko kutoka kwenye gari hilo katika kizuizi cha barabarani karibu na mji wa mkoa wa Rift Valley wa Naivasha kama kilomita 90 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi.

Kwa muijbu wa afisa mwengine wa polisi aliyekataa kutajwa jina lake mtu fulani mjini Nairobi alikuwa akiujuwa mpango huo mzima na kuwagutusha polisi baada ya gari hilo kuondoka Nairobi.