1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi nchini Afghanistani wanawasaka wauaji wa waandishi wa habari wawili wa Deutsche Welle

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4G

Waziri wa mambo ya ndani wa Afgahanistani amesema kwamba hawajafanikiwa kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya waandishi wa habari wawili wa Radio hii ya Deutsche Welle katika eneo hilo. Karen Fischer na Christian Struwe walipatikana wameuawa kwa kupigwa risasi katika mkoa wa Baghlan. Deutsche Welle ilisema waandishi hao wawili walikuwa wakifanya utafiti kwa shughuli zao za kibinafsi. Jana, wafanyakazi wa Radio Deutsche Welle mjini Bonn, waliomboleza kifo cha wenzao hao wawili. Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Erik Bettermann, alisema kuwa Deutsche Welle itaendelea kusaidia katika ukarabati wa Afghanistani katika kuwatendea haki wafanyakazi hao waliouawa.