1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antrittsbesuch des Bundespräsidenten Gauck in Polen

27 Machi 2012

Rais mpya wa Ujerumani, Joachim Gauck, ameanza ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie madarakani kwa kutua mguu wake nchini Poland, ikiwa ni kuonesha kwake imani aliyonayo na nchi hiyo ya mashariki.

https://p.dw.com/p/14T4m
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto) na mwenyeji wake, Rais Bronislaw Komorowski wa Poland.
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto) na mwenyeji wake, Rais Bronislaw Komorowski wa Poland.Picha: picture-alliance/dpa

Ikiwa Joachim Gauck ndio rais mpya, basi Wapoland wanajisabilia. Tangu alipozungumzia mjini Warsaw kuhusu "chimbuko la uhuru barani Ulaya" lililomkaa sana moyoni. Lakini hata bila ya matamshi hayo ya dhati,Gauck si mgeni mjini Warsaw. Anaenziwa sana kutokana na jukumu lake la zamani kama mkuu wa idara inayochunguza visa vya upelelezi vya Ujerumani Mashariki ya zamani, Stasi.

Rais Bronislaw Komorowski aliutaja uamuzi wa Gauck wa kuichagua Poland kufanya ziara yake ya kwanza nchi za nje kuwa ni " ishara muhimu." Ni ishara inayoonyesha kwamba uhusiano wa pande mbili kati ya Ujerumani na Poland umepindukia "suluhu ya kawaida".

Gauk pia amesisitiza "kukutana kwao kumekiuka kizingiti cha zamani cha mtengano na kujongelea karibu zaidi maadili yanayowaunganisha wananchi wa pande mbili."

Gauck na Komorowski wamehakikisha wamepania kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya Ujerumani na Poland,kama alivyokua amepania kuundeleza mtangulizi wake Christian Wulff. 

Kutangulizwa mbele vijana

Mnamo siku za mbele marais hao wawili wanapanga kutanguliza mbele Ulaya na kupigania kwa pamoja juhudi za kulileta pamoja bara la Ulaya.Sio tu umoja wa ulaya,bali hata nje zilizoko nje ya mipaka yake.Wanasiasa wote wawili wanataka kupigania uhuru na demokrasia zaidi na hasa nchini Byelorussia na Ukraine.Gauck amesifu msimamo wa Poland kuelekea Umoja wa Ulaya  pamoja na kuunga mkono sera za kuleta utulivu.

Rais Gauck akikaribishwa na mwenyeji wake, Rais Komorowski.
Rais Gauck akikaribishwa na mwenyeji wake, Rais Komorowski.Picha: picture-alliance/dpa

Hata hivyo marais wote hao wawili wameweka wazi kabisa,hawatoyaacha kando yaliyotokea zamani.Inamaanisha kwamba Joachim Gauck na  Bornislaw Komorowski watadhamini kwa pamoja uongozi wa taasisi ya vijana wa Ujerumani na Poland.

Zaidi ya hayo wanataka kuendeleza midahalo pamoja na vijana na ndio maana hivi karibuni watashiriki katika majadiliano,katika kituo cha vijana mjini Kreisau/Krzyzowa na katika chuo kikuu cha Viadrina mjini Frankfurt an der Oder.Khusu uhusiano wa pande mbili, Komorowski anasema mengi yameweza kupatikana,hata hivyo kuna baadhi yanayohitaji kutekelezwa.

Wapoland wanafurahi kwamba Gauck ameitaka nchi yao kuwa mfano mzuri kwa Wajerumani. "Kipindi chote cha maisha yangu Wajerumani wamekuwa wakliangalia magharibi." Amesema na kuongezea hamu yake ni kuona upeo wa macho wa wajerumani wenzake ukiwa mpana zaidi kuelekea mashariki.

"Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa majirani zetu wa Poland." amesisitiza Gauck akiwa mjini Warsaw.

Asifiwa kwa mchango wake

Kile ambacho wapoland wengi kinawavutia kutoka kwa Joachim Gauck ni ile namna yake ya kuzungumza kwa dhati kuhusu halai ya majirani, tangu kinachotenganisha mpaka kile kinachounganisha.Akiwa mpintzani wa zamani wa Ujerumani Mashariki ya zamani GDR, akiwa mtu mwenye kutafakari na muumini wa kikristo,amefanikiwa kuwafanya wapoland watambue kwamba kweli anawaelewa.

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto) na mwenyeji wake, Rais Bronislaw Komorowski wa Poland.
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto) na mwenyeji wake, Rais Bronislaw Komorowski wa Poland.Picha: Reuters

Inahusiana na mada moja ambayo inazusha mabishano nchini Poland: jinsi ya kutafakari yaliyopita wakati wa utawala wa kikoministi. Wengi wa Wapoland wanamjua Joachim Gauck kama mtu aliyepigania uhuru na haki na kama mkuu wa idara ambayo nchini Ujerumani ilijishughulisha na kutatahmini maovu ya utawala wa zamani wa GDR.

Kile ambacho Gauck alifanikiwa wakati ule kukifanya katika Ujerumani iliyoungana, kimewezekana nchini Poland miaka karibu 10 baadaye. Palihitahjika muda wote huo kuweza kuunda idara kama hiyo. Mpaka leo lakini inabishwa.

Wapoland wanamuangalia Gauck kwa hishma na matumaini mema. Anaangaliwa kama mtu na kama mkuu wa idara kama hiyo ya kusaka ufumbuzi kwa misingi ya Kikristo: kwa upande mmoja kuujua ukweli na kwa upande wa pili kuwa na moyo wa Kikriso kuweza kusamehe.

Na hivyo pia ndivyo Wapoland wengi wanavyohisi, wanapoisifu ziara ya kwanza ya Joachim Gauck nchi za nje.

Mwandishi: Rosalia Romaniec
Tafsiri: Hamidou Oummilkheir
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman