1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PHUKET:Thailand yasema rubani angeweza kuepuka ajali

Maafisa wa usalama wa anga nchini Thailand wamesema kuwa rubani wa ndege iliyopata ajali siku ya jumapili alipata ruhusa ya kutua muda mfupi tu kabla ya ajali hiyo iliyoua watu 89.

Wamesema kuwa ndege mbili zilizotua muda mfupi kabla ya ndege hiyo zilitoa taarifa ya hali ya upepo mkali kitu ambacho rubani angeweza kukiepuka.

Waziri wa usafiri wa Thailand amewataka wananchi kutohukumu kabla ya uchunguzi kukamilika.

Taarifa za safari za ndege hiyo zinatarajiwa kupelekwa Marekani na majibu yanatajiwa mnamo ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com