1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR: Shambulizi la bomu limeua watu 7

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx3

Bomu lililotegwa ndani ya gari limeripuka kwenye uwanja wa kuegeza magari karibu na Mahakama Kuu, mjini Peshawar,kaskazini-magharibi mwa Pakistan. Kwa mujibu wa polisi,hadi watu 7 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni raia waliokuwa wakipita njia. Mripuko huo umetokea majuma mawili baada ya mwanamgambo aliejitolea muhanga kujiripua kwenye mkahawa na kusababisha vifo vya watu 25.Maafisa wa usalama walisema,shambulizi hilo huenda ikawa lilifanywa kulipiza kisasi kuuawa kwa mkuu wa kijeshi wa Taliban,Mullah Dadullah siku chache kabla ya hapo katika nchi jirani ya Afghanistan. Hiyo ni ishara nyingine kuwa vita kati ya wanamgambo wa Kitaliban na vikosi vya Shirika la kujihami la nchi za Magharibi NATO nchini Afghanistan,vinavuka mpaka na kuingia Pakistan.